Wednesday 12 February 2025 - 16:19
Mkutano wa Wanasayansi, Wataalam na Maafisa wa Tasnia ya Ulinzi ya nchi na Kiongozi wa Mapinduzi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi katika kikao na Wanasayansi, Maafisa na Wataalamu wa sekta ya ulinzi, akisisitiza kuendelea kwa ubunifu wa maendeleo ya ulinzi, ameyataja matembezi ya mwaka huu ya tarehe 22 Bahman (Februari 10) kuwa ni vuguvugu la Wananchi na harakati kubwa ya kitaifa chini ya mashambulio ya vyombo vya habari vya adui, na akathamini na kuonesha shukurani zake kwa wananchi akisema: Taifa limepigia kelele za Umoja wake na kuonyesha utambulisho, utu, nguvu na uthabiti wa Wairan dhidi ya vitisho vya mara kwa mara vya adui.

Shirika la habari la Hawza - Kabla ya Mkutano huu, Amiri Jeshi Mkuu Ayatollah Khamenei alitembelea Maonyesho ya Nguvu (Uwezo) ya mwaka 2025 (1403 Shamsiyyah) kwa saa moja, ambayo yalijumuisha mafanikio na (nguvu) uwezo wa hivi karibuni wa Wanasayansi na Wataalamu katika Tasnia ya Ulinzi ya nchi. Katika maonyesho haya, vifaa vya juu na teknolojia mpya zilizoingia katika matumizi ndani yao zilionyeshwa katika nyanja za ulinzi wa anga, makombora ya ballistic na cruise, silaha mahiri, za anga (space ammunition), Drone za (UAV ) zisizokuwa na rubani na (Aerial) angani, vyombo vya baharini na nishati.

Baada ya kutembelea maonesho hayo akiwa pamoja na Wanasayansi, Maafisa na Wataalamu wa sekta ya ulinzi, aliwapongeza kwa mnasaba wa Siku ya kuzaliwa kwa Hadhrat Baqiyatullah Al-Adham (a.t.f.s) katika siku yake ya kuzaliwa na akaiita nusu ya Sha’ban kuwa kwa hakika ni Eid ya Ulimwengu wote na ya Kibinadamu na akaongeza: “Habari njema ya uadilifu, matumaini ya kuthabiti – kuimarika kwa uadilifu na kudhihiri kwa Mwokozi ni kutimiza matakwa (matumaini) ya siku zote ya wanadamu na ya kipindi chote cha historia, na hapana shaka kuwa matakwa (matumaini) haya ya Mwanadamu yatatimia.

Ameizingatia tarehe 22 Bahman kuwa ni Eid kubwa na ya kihistoria ya Taifa la Iran na akapongeza kwa siku hii ya mageuzi, na kuongeza kuwa: Hakuna mfano katika Mapinduzi yoyote yale kwamba baada ya miaka 46 (kupita), Wananchi wakakajitokeza na kuja mitaani na kusherehekea mwaka wa Mapinduzi yao.

Kiongozi wa Mapinduzi ametaja mahudhurio ya makundi yote ya Taifa, Wanaume na Wanawake, Watoto, Wazee na Vijana katika hali ya hewa ya baridi na joto, kuwa ni vuguvugu la kitaifa na la Wananchi, na akasema: Sherehe za mwaka huu ni miongoni mwa sherehe muhimu na mashuhuri za maadhimisho ya miaka ya Mapinduzi.

Ayatollah Khamenei akikumbushia Mashambulizi ya Kipropaganda na vita laini vya hila na visivyoisha vya adui dhidi ya wamiliki wa Mapinduzi, yaani "Taifa la Iran" na dhidi ya shujaa wa 22 Bahman, yaani "Imam Khomeini (MA)", ameongeza kuwa: Katika hali kama hiyo, watu walikuja mitaani (barabarani) katika miji na vijiji vyote kwa wakati muafaka na kwa kutambua vizuri fursa na wakaeleza maneno yao na misimamo yao.

Akishukuru mahudhurio ya vijana katika maandamano ya kitaifa ya tarehe 22 Bahman amesema: Kutoka chini ya moyo wangu, ninashikamana na vijana wapendwa, na ninatumai kwamba kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu itaenea kwa Taifa hili na mustakbali mwema unangojea Taifa hili lenye hekima, ujasiri na ufahamu.

Amelitaja suala la kulindwa Taifa na Usalama wa nchi kuwa ni muhimu sana, na akasema: Nguvu ya Ulinzi ya Iran inajulikana hivi leo, marafiki wa Mapinduzi wanajivunia hilo na maadui wanaliogopa hilo, na ukweli huo ni muhimu kwa nchi.

Ameyataja maendeleo na maboresho makubwa ya kiulinzi, hasa kwa kuzingatia (hali iliyopo ya) vikwazo vinavyoendelea na visivyokuwa vya kawaida vya maadui na akasema: Hali ya sekta ya ulinzi ya Iran ni kwamba haitupi sehemu yoyote, vijana wanazalisha bora ndani. Masharti dhidi ya sekta ya ulinzi ya Iran kwamba wasitupe hata sehemu ya zana yoyote, lakini vijana (wa Iran) wanazalisha zana zilizo kuwa bora zaidi kwa ndani.

Alizingatia kufikiwa kwa safu za mbele za jeshi kuwa kunatokana na amri ya Qur'an «اَعِدّوا لَهُم مَا استَطَعتُم مِن قُوَّة» - Waandalieni nguvu (maadui) muwezavyo (Suratul-Anfal-Aya ya 60).

Yaani: Utayarifu wa hali ya juu na wenye kuendelea dhidi ya adui - na ulazima wa kuilinda nchi dhidi ya watu wenye nia mbaya, na akaongeza: Maboresho (maendeleo) yanapaswa kuendelezwa katika sekta zote za kijeshi. Kwa mfano, ikiwa tulikuwa tumeweka kiwango fulani cha usahihi kwa Makombora katika kipindi (fulani), na leo hii tunahitaji kukiongeza (kiwango hicho), hili linapaswa kufanyika.

Mwisho, Kiongozi wa Mapinduzi aliita nguvu ya mawazo (fikra), ubunifu, uvumbuzi, na uwezo wa kutafiti na kujenga kuwa ni katika baraka na neema za Mwenyezi Mungu, na zinazostahili kushukuriwa kwa moyo wa dhati, kwa kauli na vitendo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha